Ushauri wa Kisheria

Legal Advice - Swahili (Kiswahili)

Wakili anapokupa usaidizi kuhusu tatizo lako hususa la kisheria, tunaita usaidizi huo ushauri wa kisheria. Ushauri wa kisheria ni tofauti na maelezo ya kisheria, ambayo yanaweza kuwa ya jumla zaidi na kwa kawaida hutolewa na mtu anayejua sheria lakini si wakili.

Legal Aid NSW hutoa taarifa za kisheria kwa mtu yeyote aliye na tatizo la kisheria katika NSW kupitia huduma yetu ya taarifa za kisheria na ya rufaa, yaani LawAccess NSW.

Tunatoa ushauri wa kisheria bila malipo kwa njia ya simu kwa watu wanaostahiki na katika maeneo mengi katika NSW.

Utakachotarajia katika kikao chako cha ushauri

Vikao vyetu vya ushauri wa kisheria havina malipo kwako na kwa ujumla ni takriban dakika 20. Wakili atakusikiliza ukizungumza kuhusu tatizo lako, atauliza baadhi ya maswali ya kufuatilia, na kukusaidia kuamua ni nini utafanya baadaye.

Anaweza kukupa usaidizi wa hati fupi ikiwa huna wakili. Hawataweza kukusaidia kwa hati ndefu ngumu za kisheria.

Wakili wako pia atakuambia ikiwa anaweza kuendelea kukusaidia katika kesi yako. Ikiwa atafanya hivyo, wafanyikazi watakusaidia kujaza ombi la usaidizi wa kisheria.

Ikiwa hatuwezi kukusaidia zaidi baada ya kikao chako cha ushauri, tunaweza kukupa maelezo kuhusu mahali unapoweza kwenda kwa usaidizi zaidi.

Tunatoa ushauri juu ya nini

Mawakili wetu wanaweza kukusaidia katika masuala ya uhalifu yanayohusu polisi, masuala ya familia yanayohusu watoto au kuvunjika kwa uhusiano, au masuala ya kiraia ambapo unatatizika na hitaji la msingi kama vile makazi, usaidizi wa mapato au ufikiaji wa usaidizi wa afya na ulemavu.

Ni nani anayeweza kupata ushauri wa kisheria

Hatutoi ushauri wa kisheria kwa kila mtu. Kusudi letu ni kutoa huduma za kisheria kwa watu katika NSW wanaokumbana na shida, na tuna rasilimali chache za kufanikisha jambo hili.

Jinsi ya kuandaa kikao cha ushauri

Njia bora ya kujua kama tunaweza kukupa ushauri wa kisheria bila malipo au kuweka miadi ni kuzungumza na timu yetu katika LawAccess NSW.

Unaweza kuwasiliana nao kwa kupiga simu kwa 1300 888 529 au kwa kutumia huduma yao ya mazungumzo ya mtandaoni. Huwa wamefungua kutoka 9am hadi 5pm, Jumatatu hadi Ijumaa (bila kujumuisha likizo za umma).